MCHELE ulionyooka! Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti
ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’ na mchumba’ke, Nangari
Kombo wanadaiwa kutibuana, kisa kikidaiwa ni maneno ya wanafiki
yasiyokuwa na ukweli.
Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’
Habari za chini ya kapeti zilinyetisha kwamba mtiti kati ya wawili
hao ulijiri juzikati baada ya Kombo kudaiwa kuanza kumtuhumu Linah kuwa
anapokuwa kwenye ziara za matamasha kama Fiesta huwa anamsaliti na
wanaume wengine.
Lina akiwa na mpenzi wake, Nangari Kombo.
Chanzo hicho kilidai kwamba, kufuatia madai hayo Kombo alimuanzishia
Linah bonge la tafrani na kujikuta kila mmoja anachukua hamsini zake.
Linah alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Ni kweli kulitokea kutoelewana but (lakini) tumeyamaliza, tupo vizuri sana.”
No comments:
Post a Comment