Baada
ya watanzania na wadau wengi wa urembo na mitindo nchini kukinukisha
kwa kuukataa ushindi wa Sitti Mtemvu kuvikwa taji la Miss Tanzania 2014
kwa madai hakuwa na sifa na ana umri mkubwa sasa kimenuka !...
Habari
ambazo zimeandikwa leo mpaka magazetini ni kuwa kuna uwezekano mkubwa wa
Sitti kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014 huku issue ya umri wake ikiwa
moja ya point kuu za kumvua taji hilo. Inadaiwa pia kuwa kwasasa
wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania wamegawanyika ambapo kuna
wasioukubali ushindi wa Sitti huku wengine wakiona sawa tu.
Habari
zaidi zinadai kuwa kamati na waandaaji wa Miss Tanzania wanataka kumvua
Sitti taji ili kuendelea kuweka taswira, imani na usafi wa shindano hilo
kwa kuondoa kashfa ya upendeleo na rushwa kama ilivyo midomoni mwa watu
kuhusu shindano hilo kwasasa baada y aSitti kukataliwa kuwa Miss
Tanzania 2014. Pia inadaiwa kuwa kamati ya Miss Tanzania ina hou na
issue ya Sitti kufika kwa waandaaji wa Miss World na hivyo kuweza
kulizuia shindano la Miss Tanzania miaka kadhaa au kufuta ushiriki wao
kabisa.
Inadaiwa
kuwa ikiwa Sitti atavuliwa taji basi kuna uwezekano mkubwa Jihan
Dimmachk akaiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2015
kutokana na watanzania wengi kumkubali na kudai ameonewa kuliko hata
mshindi wa pili Lilian Kamazima.
Vigezo
vinavyolalamikiwa kumpa ushindi Sitti ni utata wa umri wake huku wazazi
wake mama akisema mwanae ana miaka 29 wakati baba mzazi na Sitti
mwenyewe wakisema ana mika 18 huku passport yake ikionyesha ana miaka
25, umbo lake anadaiwa kuwa mnene hivyo kukosa sifa za umiss, anadaiwa
kuwa na mtoto wa miaka 6-8, swali hakujibu vizuri huku akichanganya na
lugha ya kifaransa ambayo awali hakuichagua, inadaiwa kuwa sifa zake
hazikumzidi Jihan na Lilian Kmazima walioshika nafasi za pili na tatu.Jihan
Jihan Dimachk ambaye watanzania na mashabiki wengi wa urembo wamelalamikia kuwa ameonea yeye ndiye alistahili kupewa taji
No comments:
Post a Comment