Tukio hilo
lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack
alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana
maraha.Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka
kwenda katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha
rafiki yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Mume
aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar,
amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack
wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana
miezi miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika
nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi
ambapo watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
"Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia
lakini kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya
mumeweambaye anakuwa amekwenda kazini," alisema mmoja wa wapangaji wa
nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha
Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika
chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na
mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo
kwenda kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti
za kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni,
Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia 'mchezo'
ukiendelea chumbani Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia
mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na
kutonywa kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa
rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi
milioni 1.2 ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa
shilingi laki mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa
askari mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa
ajili ya hatua zaidi za kisheria.
No comments:
Post a Comment