T.I akiwa na manager wake Jason Geter
Ikiwa ni
siku chache tu zimebakia ili shangwe za Serengeti Fiesta zitawale katika
maskio ya wakazi wa Dar es Salaam, October 18, Meneja wa T.I., Jason
Geter pamoja na meneja wa Wizkid na Waje, Cecil Hammond, wanatarajia
kutoa semina kwa wadau wa muziki itakayofanyika ijumaa hii. Akizungumza
Mtandao huu leo
mwenyekiti
wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Sebastian Maganga, amesema meneja
wa T.I. na yule wa Waje wanatarajia kuingia Jumatano, October 15 ili
kujiandaa na shughuli mbalimbali ikiwemo semina pamoja na kufungua duka
litakalouza kazi za T.I.
“Mpaka
sasa ratiba inaenda vizuri, meneja wa T.I ‘Jason Geter’ na meneja wa
Waje na Patoraking, wanatajia kuingia usiku wa Jumatano, kwa sababu kama
meneja wa T.I. anakuja mapema ili kuangalia mazingira na atakuwa na
semina na wadau wa muziki kuzungumzia jinsi muziki au msanii unavyoweza
kutumia jina lako kibiashara. Pia atafungua duka ambalo litakuwa linauza
productiob za T.I. Pia meneja wa Waje ‘Cecil Hammond’ atakuwepo kwenye
semina hiyo,” alisema Sebastian Maganga.
Cecil Hammond
Pia
Sebastian alisema wasanii wa kimataifa wanaotarajia kupagawisha kwenye
jukwaa la Serengeti Fiesta ni T.I, kutoka Marekani, Waje na Patoraking
kutoka Nigeria pamoja na Victoria Kimani kutoka Kenya. Pia amedai kuna
msaani mmoja mkubwa kutoka Nigeria ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na
jibu ramsi litapatikana kesho mchana.
“Katika wasanii wa kimataifa T.I. ataingia Dar Ijumaa usiku,” amesema.
Wasanii
wa Bongo wanaotarajia kupanda jukwaa moja na wakali hao kutoka nje ni,
Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Stamina, Nay wa Mitego, Vanessa
Mdee, Mwana FA, Weusi,Young Killer Msodoki, Linah Sanga, Recho, Barakah
Da Prince, Mo Music, pamoja na Super Nyota G.Luck, K. Style pamoja na
Edu Boy.
CDT:BONGO 5
No comments:
Post a Comment