Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
SHIRIKA la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga
katika baadhi ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na
wateja wake mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi
Jumatano lina habari kamili.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti
hili, baadhi ya wateja hao wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa
shirika hilo linatoa huduma ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii,
kwani tiketi zinazouzwa kwa bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa
zimekwisha.
“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi
nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba
ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri
mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini
Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet,
lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa
tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia
shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL
ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye
alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
Abiria
wakishuka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet.Alisema shirika hilo la ndege
lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa pale anapoahirisha safari au
kuchelewa ndege, tofauti na mashirika mengine kama Precision Air na Air
Tanzania.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe
tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine
humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei
aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja
hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi
wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri
mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo
akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya
mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini
muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam
tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke
wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya
ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende
nikachukue simu yangu.
Marubani
wa ndege ya Fast Jet wakiwa mzigoni.“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya
kuingia ndani ya ndege ile, badala yake wakanisaidia
No comments:
Post a Comment