JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha vikali uvumi
unaoendelea kuzushwa jijini Dar es Salaam kuhusu utekeaji nyara wa
watoto wadogo wanaosoma shule za jiji hilo na kuwataka wananchi
kuupuuza.
Akizungmza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kuwa mpaka sasa jeshi
hilo halina taarifa yoyote ya mtoto kutekwa au kufanyiwa madhara yoyote
kwa mtindo wa utekaji nyara.
“Jeshi
la Polisi limegundua kwamba huu ni uvumi ambao haujulikani chanzo chake
hivyo wananchi wanaombwa kuachana nao na kuupuza kwani unaleta hofu
katika jamii bila sababu za msingi” alisema Kova.
Alisema
kuwa pia uvumi huo umeanza kuleta usumbufu ambapo mnamo Oktoba 3 mwaka
huu saa 3:00 asubuhi huko Vingunguti, mtu mmoja aitwaye Prosper Makame
(34) akiwa na mkewe Marystella Munis (30) walipata usumbufu unaotokana
na uvumi huo.
Kamishna
Kova aliongeza kuwa watu hao ambao ni wafanyabiashara wa vyombo vya
nyumbani walifika maeneo ya shule ya msingi Kombo iliyopo Vingunguti kwa
ajili ya biashara zao, wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba T252
DAY, ghafla walizingirwa na watu wakidaiwa wanateka wanafunzi.
“Pia
mnamo Oktoba 13, 2014 majira ya saa 4:00 asubuhi huko katika kituo cha
Polisi Tabata uliibuka uvumi kuwa gari namba T548 BUN aina ya Noah rangi
nyeusi ambayo ni mali ya askari polisi A/INSP Ester wa kikosi cha
usalama barabarani, ilivumishwa kwamba ndani ya gari hiyo kuna vichwa
vitano vya watoto wa shule ya msingi Mtambani na kusababisha wazazi
wenye watoto wanaosoma shule hiyo kukusanyika kituoni hapo ili
kushuhudia na kuona vichwa hivyo” alisema Kamishna Kova na kuongeza:
“Na
ndipo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi aliamuru gari hilo lifunguliwe na
kuwathibitishia wananchi kuwa habari hizo ni za uongo na uvumi”
Kutokana
na tukio hilo jeshi hilo lilifanya uchunguzi na kumkamata mtu mmoja
Gilbert Stanley (32) mhehe mkulima na mkazi wa Tabata alipohojiwa
alikiri kueneza habari hizo na kudai yeye aliambiwa na mtu ambaye
hakumkumbuka.
Hivyo,
Kamishna Kova alisisitiza kuwa uvumi wa kuwepo kwa kikundi cha wahalifu
wanaowateka watoto wanafunzi si wa kweli hata kidogo na hivyo wananchi
wanatakiwa kuepukana na taarifa hizo kwani zinaweza kusababisha uvunjifu
wa amani.
Katika hatua nyingine,
Kamishna Kova alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu watano na wengine
16 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea Oktoba 13 mwaka huu
majira ya saa 5:00 usiku huko kwenye mzunguko wa Mbagala Charambe baada
ya lori aina ya Scania T347 BXG lilipoanguka likiwa na mafuta aina ya
petrol lita 38,000.
Aliwataja
waliofariki kuwa ni Masoud Masoud mkazi wa Charambe, Hassani Mohamed
mkazi wa Mbagala Kibangulile, Mohamed Ismail, Ramadhani Halfan na
Maulidi Rajabu wote ni wakazi wa Mbagala Charambe.
Alisema
kuwa majeruhi wamelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili na
hospitali ya wilaya ya Temeke wakiendelea na matibabu huku ajali hiyo
pia ikisababisha nyumba ya kulala wageni iitwayo United kuungua moto na
kuteketea kwa pikipiki saba za bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa karibu na
aneo hilo, maduka matano yenye bidhaa zenye thamani ya shilingi Milioni
197 yaliungua moto.
Kamishna
Kova aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukimbilia kwenye ajali za
magari ya mafuta kwani ni hatari kwa maisha yao kwani watu wengi
waliojeruhiwa walikuwa wakichota mafuta yaliyomwagika kutokanana ajali
hiyo.
Katika tukio lingine, Kamishna
Kova alisema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata jambazi sugu
aitwaye Paulo Thamas Milanzi maarufu Chinga (35) mmakonde mkazi
wa Chanika ambaye baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo
lilijeruhiwa na kufikshwa hospitali ya muhimbili kwa matibabu ingawa
baadaye alifariki dunia.
Alisema
jambazi hilo lilikuwa likitafutwa na polisi kutokan na kuhusika kwenye
matuio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa Afisa Mwandamizi wa
Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29 mwaka huu liliotokea
Uwanja wa Ndege.
Aliongeza
kuwa jambazi lilikamatwa na bastola aina ya Star ambapo majambazi
wenzake walikamatwa na sasa wako gerezani, hivyo ameitahadharisha jamii
iachane na uhalifu kwani hauna manufaa yoyote.
No comments:
Post a Comment