Stori: Erick Evarist
FEDHA haina
mwenyewe! Siku chache baada ya kudaiwa kuyumba kiuchumi kiasi cha
kuzidiwa jeuri na aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’, Beautiful
Onyinye, Wema Sepetu ameibuka na kujibu mapigo kwa kumwaga ‘mafedha’
ukumbini, Risasi Mchanganyiko linashuka na mzigo kamili.
Wema akimwaga manoti kwa mwimbaji wa Skylite Band.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilichukua nafasi Ijumaa
iliyopita katika Ukumbi wa Thai Village, Masaki jijini Dar kulipokuwa na
sherehe maalum ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa vinywaji vikali vya Jack
Daniel, Mr. Jack’s.
WEMA ALIUMIA MOYONI
Chanzo kilicho karibu na
Wema, kilipenyeza habari kuwa, msanii huyo hakufurahishwa na kitendo cha
watu kumuona kafulia kiasi cha kuzidiwa na K ambaye aliwahi kumlipia
faini ya shilingi mil. 13 kumnusuru na kifungo cha miaka mitano jela.
KIFUNGO KILIKUWAJE?
Kajala alikuwa anakabiliwa
na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa
na tuhuma za kutakatisha fedha haramu.Wema akizidi kumwaga manoti kwa mwimbaji huyo.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Wema hakufurahishwa na
kitendo cha watu kumsemasema kila siku kwamba kafulia, hakupenda
kuambiwa kazidiwa fedha na K wakati anaamini bado fedha anazo sema
aliamua kukaa kimya kwani hakupenda majibizano ya kwenye vyombo vya
habari,” kilisema chanzo hicho.
JEURI YAANZIA TEN LOUNGE
Awali, mwanahabari wetu
alimshuhudia Wema akiwa na wapambe wake katika Ukumbi wa Ten Lounge
(zamani Business Park) uliopo maeneo ya Victoria, Makumbusho jijini Dar
ambapo alifika kushuhudia burudani za wasanii mbalimbali.
RAUNDI ZAZUNGUSHWA
Akiwa ukumbini hapo, wapambe
wake walionekana kutumia vinywaji mbalimbali (vilivyo na visivyo na
kilevi) huku mwenyewe naye akitumia mvinyo wake ambao kwa macho ya
kawaida unaonekana si wa pesa za mawazo.
FULL KUREKODIWA
Kuonesha kwamba fedha ipo, kila
tukio alilokuwa akilifanya Wema na wapambe wake ukumbini hapo, lilikuwa
likirekodiwa na mtu maalum waliyekuja naye na kisha kuondoka pamoja.Pesa aliyotunzwa mwimbaji huyo na wema.
THAI VILLAGE SASA
Baada ya kutumia vya kutosha
Ten Lounge, msururu wa Wema ulihamia katika Ukumbi wa Thai Village
ambako ndipo jeuri ya fedha ilipokwenda kukamilika.
Chanzo makini
kilichokuwepo ukumbini humo kilimwaga data kwamba, Wema alifika akiwa na
kundi la wapambe wake na kwenda kukaa mahali kwa muda huku raundi za
vinywaji zikizungushwa kwa staili ya kata mti, panda mti.
AKUNWA NA MUZIKI WA SKYLIGHT
Wakati Miss huyo
asiyechuja tangu alipotwaa taji hilo mwaka 2006 akiendelea kupata
vinywaji vya hapa na pale, muziki mzuri wa Skylight Band ulimuinua na
kujikuta yupo jukwaani chini ya himaya ya mwanamuziki mahiri
anayefahamika kwa jina la Sam Mapenzi.
“Sam alimpagawisha kinoma Wema pale alipopiga wimbo wa All of Me
ulioimbwa na John Legend, mtoto wa kike akapanda jukwaani na kukaa
karibu yake, akawa anasikiliza mashairi hayo huku akimwaga manoti ya
hatari katika kumtunza,” kilisema chanzo hicho.
ZAMZIDI KAJALA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka
kuwa, kwa hesabu za harakaharaka, Wema alimwagia Sam noti za elfu
kumikumi zisizopungua mia moja (jumla milioni moja) hivyo kuzipiku zile
za Kajala alizomwaga hivi karibuni wakati akiwatunza Yamoto Band katika
Viwanja vya Leaders zilizodaiwa kufikia shilingi laki saba.Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Beautiful Onyinye, Wema Sepetu.
“Chezea Madam (Wema) wewe, kamwaga pesa kama hana akili nzuri, alitoa
pochi ndogo iliyokuwa ndani ya pochi kubwa, balaa.“Zile alizotoa Kajala
kwa Yamoto Band zilikuwa fedha za mboga, Madam kamwaga fedha ya maana
leo,” kilisema chanzo hicho.
MPAMBANO UNAENDELEA?
Baadhi ya wadau wa burudani
waliozungumza na mwandishi wetu, walidai Kajala hawezi kukubali
kuzidiwa, hivyo lazima naye atasababisha tukio la maana hivi karibuni.
“Unafikiri Kajala atakubali? Subirini mtaona jeuri yake hivi karibuni,” alisema mdau huyo huku akiomba hifadhi ya jina.
TUJIKUMBUSHE
Makabrasha ya Risasi Mchanganyiko
yanaonesha kwamba, Wema na Kajala walikuwa marafiki wa kushibana lakini
baadaye walipishana kauli na sasa kila mmoja anaishi kimpango wake.
No comments:
Post a Comment