Stori: Shani Ramadhani
MWANADADA
anayefanya poa katika tasnia ya filamu za Kibongo Salma Jabu ‘Nisha’
hivi karibuni alilazimika kuwachezea wanafunzi waliomtaka kufanya hivyo
wakati wao wakimuimbia katika maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam.
Mwanadada anayefanya poa katika tasnia ya filamu za Kibongo Salma Jabu ‘Nisha’.
Akizungumza na gazeti hili, Nisha alisema aliteremka kwenye gari kwa
ajili ya kuuliza sehemu aliyokuwa anataka kwenda, ghafla wakajitokeza
vijana hao ambao ni mashabiki wake waliomtaka akate kiu yao.
“Ile kushuka ili niulizie sehemu nikashangaa kundi la wanafunzi
limenivamia na kuanza kuniambia Nisha shuka huku wakiimba na kunitaka
niwachezee, ikanibidi nifanye wanavyotaka baada ya hapo wakanielekeza
nikaondoka, kiukweli nilifurahi na napenda sana kuona mashabiki zangu
wakinipa sapoti,” alisema.
No comments:
Post a Comment