Ofisa
Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
(kushoto) akizungumza na wanahabari mara baada ya mkutano wa wadau wa
mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL. Kushoto kwake ni Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January MakambaOfisa
Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
(kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam.Ofisa
Masoko wa Mauzo ya Jumla wa TTCL, Gipson Mosha akitoa maelezo kwa
wanahabari (hawapo pichani) juu ya huduma mpya ya uuzaji wa interneti
'IP Pop -Internet Protocol Point of Presence' iliyoanzishwa na kampuni
hiyo.Ofisa
Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akitoa
maelezo kwa baadhi ya wadau wa mawasiliano waliotembelea meza ya kampuni
hiyo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano wa Afrika Mashariki na
Afrika kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mratibu wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Anifa Chingumbe (kushoto) akitoa
maelezo kwa baadhi ya wadau wa mawasiliano waliotembelea meza ya kampuni
hiyo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano wa Afrika Mashariki na
Afrika kwa ujumla leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
(kushoto) akizungumza katika mdahalo wa wadau wa mawasiliano uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wadau washiriki katika mkutano wa wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo kampuni ya TTCL wakifuatilia mkutano huo.
KAMPUNI
ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imeanzisha kituo cha kuuzia huduma za
interneti 'IP Pop -Internet Protocol Point of Presence' nchini ikiwa ni
jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano zaidi. Huduma kama hii awali
ilikuwa ikinunuliwa nje hasa makampuni anuai yanayotoa huduma hizo
barani ulaya.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota alipokuwa akizungumza na
wanahabari katika mkutano wa wadau anuai wa mawasiliano kutoka nchi za
Afrika Mashariki na baadhi za mataifa ya Afrika unaofanyika Tanzania.
Ngota alisema kampuni ya TTCL imekuwa na mchango mkubwa wa kusimamia
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuwawezesha Watanzania na hata nchi
jirani kupata mawasiliano mazuri kutoka katika nchi zao hadi katika nchi
za ulaya.
"...Kuna
juhudi mbalimbali TTCL tunafanya ili kuongeza fursa kwenye mawasiliano
ambapo kwa sasa tumefungua kituo cha kuuzia interneti hapa nchini,
kinaitwa IP Pop (Internet Protocol Point of Presence). Awali interneti
tulikuwa tunaenda kununulia London kwenye makampuni mbalimbali sasa hivi
tumeanzisha kituo chetu cha kununulia intaneti hapa hapa nchini...Kwa
hiyo tunawakaribisha watumiaji wa interneti kuja kununua huduma hizi
kwetu," alisema Ngota.
Akizungumzia
mkutano huo, Ngota alisema wadau wa mawasiliano Afrika ikiwemo TTCL
imejipanga vizuri kutumia fursa ambazo zinaweza kupatikana nchini na nje
ya nchi ili kuendeleza sekta ya mawasiliano. "...Unapopiga simu lazima
uende hadi nchi za nje kupata ile njia alafu ndo unarudi ulipo Afrika
sasa hivi tunaangalia namna gani tutajikwamua na huduma kama hizo
kuzipata hapa hapa Afrika..." alisema ofisa huyo wa TTCL.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba akizungumzia mkutano huo alisema mkutano huo ni muhimu kwani
wadau wa mawasiliano wamekutana kujadili maendeleo ya sekta ya
mawasiliano, hasa katika ukanda wa afrika mashariki na afrika kwa
ujumla. Alisema Tanzania inategemewa sana na nchi karibia saba ambazo
zipo pembezoni mwa bahari kupitia huduma ya mkongo wake wa mawasiliano.
"Mkongo
wa mawasiliano wa kimataifa umetua katika bahari yetu na sisi tunauza
huduma hiyo kwa nchi nyingine...Tumeupeleka hadi kwenye mipaka ya
majirani zetu kama Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na wengineo ambao
hawana mawasiliano."
Makamba
alisema mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata
mawasiliano mazuri na yalio bora maana hiyo ni haki yake. Sera na kanuni
za Serikali ni kuhakikisha hilo linafanikiwa. Aliongeza kuwa kwa
kulitambua hilo Serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kujenga
mkongo wa taifa wa mawasiliano.
"..Na
sasa tunaingia kwenye awamu ya tatu ya upanuzi wa mkongo huo ikiwa ni
sambamba na uboreshaji wa mawasiliano, ili ufike kila wilaya nchini,
Watanzania wengi maeneo ya vijijini bado hawana mawasiliano, sehemu
nyingine hakuna mawasiliano kabisa au pengine yapo lakini si mazuri.
Aidha
alibainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015
maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yanapata mawasiliano, hii ni
pamoja na kukaribisha makampuni mapya yaweze kuwekeza katika sekta hii
ili uwepo ushindani kwamba kama kuna maeneo kampuni fulani haitaki
kwenda basi nyingine ziende huko.
"...Mkongo
wa taifa wa mawasiliano ni biashara na majirani zetu wanategemea na
wananunua huduma hiyo kutoka kwetu. Tunachokifanya ni kuiimarisha
kampuni ya TTCL hadi sasa wanafanya kazi nzuri sana wana wadau na
washirika wengi toka nchi jirani ambapo wanafanya nao biashara. Kazi ya
Serikali ni kuiwezesha ili biashara hiyo iwe kubwa zaidi," alisema
Makamba.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment