Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa
nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi
kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo ya Msanii bora
wa mwezi wa kituo cha televisheni cha MTV Base kinachorusha matangazo
yake kutoka Afrika Kusini na kuyafikia maeneo mengi duniani.
Aidha,
Baraza linampongeza msanii huyu na wenzake Peter Msechu na Vannessa
Mdee kwa kuchaguliwa kushindania tuzo mbalimbali katika tuzo za “All
Africa Music” (Afrima) ambapo nyimbo zaidi ya 2025 kutoka kwa wasanii
mbalimbali barani Afrika zinatarajiwa kushindanishwa na washindi
kupatikana.
Kuteuliwa
na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo mbalimbali za Afrika na
duniani ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na nje ya
Tanzania.
Baraza
linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu,
bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze
kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la
kulitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Ni
matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa
kufuata sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment