Hospitali moja mjini Fanakfurt
Ujerumani inamtibu mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa nchini humo nyakati za
usiku chini ya ulinzi mkali.
Baada ya kuwasili kwa ndege kutoka
Afrika Magharibi, mwanamume huyo alifikishwa katika hospitali ya
Frankfurt University ambako aliwekwa karantini.Mwanamume huyo ni daktari kutoka Uganda ambaye aliwatibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone.
Hiki ni kisa cha pili cha mgonjwa wa Ebola kupatikana Ujerumani. Kisa cha kwanza kilikuwa cha mwanamume aliyewasili mjini Hamburg akiwa na Ebola kutoka Afrika Magharibi mwezi Agosti.
Katika kanda ya Afrika Magharibi, zaidi ya watu 3,338 wamefariki kutokana na Ebola ukiwa mlipuko mbaya zaidi wa Ebola kuwahi kushuhudiwa duniani.
Watu 7,178, walithibitishwa kuwa na Ebola nchini Sierra Leone, Liberia na Guinea ikiathirika zaidi kuliko nchi nyinginezo.
Madaktari katika hospitali hiyo wamesema kuwa mgonjwa huyo ameshughulikiwa vyema.
No comments:
Post a Comment