Samahani ndugu wasomaji kwa picha hizi,mwili wa marehemu Merkion Mgimba(Msuruisi) ukiwa katika eneo la tukio
majirani wakiuangaliwa mwili wa marehemu Mgimba
Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Merkion Mgimba(Msuruisi) miaka
70 mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe
ameuawa kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28 oktoba
2014 akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga
alisema kuwa marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la
kujisaidia haja ndogo lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake
na kuanza kupambana naye ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani
akipiga kelele.
Bi.Theodora alisema baada ya kusikia kelele hizo sebuleni alilazimika
kutoka chumbani ili aende kutoa msaada kwa mumewake lakini alipofungua
mlango wachumbani alikutana na nondo iliyompata mkononi ndipo alipofanya
uamuzi wa kutokea dirishani ili aende kuomba msaada lakini juhudi hizo
hazikuzaa matunda kwani alishuhudia mtu aliyevalia shati jeupe
akitokomea gizani.
Alisema baada ya muuaji huyo kukimbia alirudi kuona hali ya mumewe
lakini alimkuta tayari ameshaaga Dunia,hapo akachukua uamuzi wa kwenda
kuwaeleza majirani na kiongozi wa mtaa ili kumsaka muuaji huyo ambaye
hakuweza kumfahamu zaidi ya kushuhudia shati lake jeupe.
“Nilisikia mumewangu akikimbia kutoka nje na baadae kelele sebuleni
ndipo nilipotoka ili kutoa msaada lakini nilipofungua mlango wa chumbani
muuaji huyo alinipiga na nondo mkononi ikanilazimu kufunga mlango na
kurudi chumbani nikisikia mume wangu akilia kwa uchungu,nikaamua kupitia
dirishani ili niombe msaada kwa majirani ndipo nilipomuona muuaji huyo
akikimbia kichakani”,Alisema Bi.Theodora.
Alisema muuaji huyo hajachukua kitu chochote zaidi ya kufanya
mauaji,pia alithibitisha kuwa hii ilikuwa ni awamu ya pili kwani
kunakipindi marehemu aliwahi kupambana na mtu nje ya nyumba yake nyakati
za usiku na kumshinda mtu huyo alibeba nondo kama ilivyokuwa leo ila
hakutambulia.
Aidha kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani
amethibitisha kutokea tukio hilo alisema mpaka sasa bado jeshi la
polisi linaendelea na upelelezi wake ili kumbaini muujia taarifa kamili
zitatolewa upelelezi ukikamilika.
Mwisho.
- See more at:
http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/10/auawa-kwa-kupigwa-nondo-wilayani-ludewa.html#sthash.kRaihi9O.dpuf
No comments:
Post a Comment