Wanahabari mbalimbali wakimsikiliza Wambura.
...akiwa na wanahabari.
SHIRIKISHO la Soka Nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Azam Fc dhidi ya washindi wa pili wa ligi hiyo Yanga SC .
Mchezo huo ni wa kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2014/15 unatarajiwa kupigwa Jumapili ya Septemba 14 kwenye dimba la Taifa jijini Dar kuanzia majira ya saa10:00 alasiri.
Akizungumza na GPL Kaimu katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura amesema wameamua kupanga viingilio vya bei nafuu ili kuwapa fursa watazamaji wa hali ya chini kuweza kuvimudu.
“Viingilio ni Sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, 10,000 viti vya rangi ya chungwa, 20,000 V.I.P B na S na 30,000 kwa V.I.P A, unaweza kununua kwa M-Pesa, maduka ya Fahari Huduma pamoja na CRDB Simu Banking.
“Siku hiyo pia kutakuwa na zoezi la kuchangia damu salama na watu 70 wa mwanzo watakaochangia watalipiwa tiketi za kukaa V.I.P B na C” alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment