Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo
aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri
zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.
“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la
kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia
ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:
“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini
siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu
ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.
No comments:
Post a Comment