Kila kukicha kunaibuka vituko vingi duniani, wamo wanaosema huenda ni
mwisho wa dunia! Mama mmoja almaarufu kwa jina la Mama la Mama anadaiwa
kumbonda hawara wa mumewe baada ya kumwekea mtego wa fumanizi kwenye
nyumba ya kulala wageni (gesti).Hawara akihaha ndani ya gesti ya White
Paris (kimara) mara baada ya fumanizi. SEKESEKE
Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari
wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo
eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na
kufunga mtaa.
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo
aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya
simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe
alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
Hawara
akidhibitiwa mara baada ya kunaswa katika mtego wa Mama la mama.
Ilidaiwa kuwa baada ya mumewe kuondoka na simu bila kujua haina laini,
Mama la Mama aliiweka laini hiyo kwenye simu yake kisha akapitia namba
kadhaa na kuitilia mashaka moja na alipopiga, akawa amepatia.Akamhadaa
kwa kubadilisha sauti na kuzungumza kama mumewe.
MWANAMKE AINGIA MKENGE
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa
kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni
‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.
Hawara
akipokea kichapo hevi kutoka kwa Mama la mama. Ilielezwa kwamba Mama la
Mama alimdanganya hawara huyo kuwa endapo wataonana atapona hivyo
akamwambia wakutane gesti hiyo kwa kuwa Mama la Mama ni mkazi wa Kimara,
Dar.Ilisemekana kuwa Mama la Mama, huku akijifanya mwanaume alimuomba
hawara huyo wakutane gesti kwani alikuwa amekumbuka penzi lake.
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka,
akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za
kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda
kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye
alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.
Hawara akitoka gesti mara baada ya kuambulia fedheha kuu iliyomsibu. NDANI YA CHUMBA CHA GESTI
Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa
ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake
ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa
amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa
ndani na nje ya gesti.
KIPONDO
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba
amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.
Hawara kulia akiwa mapokezi ya gesti hiyo. HAWARA AKODI CHUMBA KUKWEPA KIPIGO
Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti
akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa
wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama
chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala. Akiwa kwenye mishemishe
zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana
aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke
aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa
kwani ni baamedi.
Umati wa watu ulioshuhudia laivu songombingo hilo. MTUHUMIWA ANENA
Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa
Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi
kwa takribani mwezi mmoja.
Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Hadi gazeti hili linang’oa nanga eneo la tukio Mama la Mama alikuwa
ameondoka eneo hilo huku hawara akiendelea kutandika usingizi chumbani.
No comments:
Post a Comment