Dar es Salaam, Jumanne 07 Octoba 2014: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za mitumbwi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu wa 2014. Mashindano haya ya “kupiga makasia” yanafanyika kwa mwaka wa kumi na tano sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”. Alisisitiza pia umuhimu wa michezo katika kujenga afya bora.
Edith alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya mitumbwi yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa kama ratiba inavyoonyesha hapo chini kwa hatua ya awali.
TAREHE | MAHALI/MKOA | UWANJA |
18/10/2014 | KIGOMA | UFUKWE WA MAGEREZA |
01/11/2014 | BUKOBA | UFUKWE WA SPICE BEACH |
08/11/2014 | MWANZA | UFUKWE WA MWALONI |
15/11/2014 | KISIWA CHA UKEREWE | UFUKWE WA HOTELI YA MONARCH |
22/11/2014 | MUSOMA | UFUKWE WA BWALO LA POLISI |
Edith Bebwa akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI | NGAZI YA MKOA WANAUME | NGAZI YA MKOA WANAWAKE | NGAZI YA KANDA WANAUME | NGAZI YA KANDA WANAWAKE |
Mshindi wa Kwanza | 900,000 | 700,000 | 2,700,000 | 2,300,000 |
Mshindi wa Pili | 700,000 | 600,000 | 2,300,000 | 1,700,000 |
Mshindi wa Tatu | 500,000 | 400,000 | 1,700,000 | 900,000 |
Mshindi wa Nne | 400,000 | 300,000 | 900,000 | 700,000 |
Mshindi wa 5 – 10 | 6 @ 250,000 | 6 @ 200,000 | 6 @ 400,000 | 6 @ 250,000 |
No comments:
Post a Comment