SURUA
na rubella ni magonjwa hatari yanayoenezwa haraka kwa njia ya hewa,
kutoka kwa mtu mwenye vimelea vya ugonjwa huo kwenda kwa mwingine.
Wataalamu
wa afya wanaeleza kuwa dalili za magonjwa haya mawili zinafanana, hivyo
ni vigumu kutofautisha. Wataalamu hao wanasema dalili kuu ni homa na
vipele vidogovidogo.
Chanjo
ya surua-rubella hutoa kinga kamili dhidi ya magonjwa haya. Dozi ya
kwanza hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 na dozi ya pili
akiwa na mwaka mmoja na nusu (miezi 18).
Serikali
kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imekutana na wadau wake wa
masuala ya chanjo jijini Dar es Salaam jana, kuzungumzia mkakati wa
kampeni za chanjo ulio na lengo la kuwafikia walengwa wengi zaidi ili
kuongeza idadi ya watu wenye kinga dhidi ya magonjwa ya surua na
rubella.
Endelea kusoma zaidi hapa : FATHER KIDEVU BLOG
No comments:
Post a Comment