Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta
yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es
salaam.
Taarifa
iliyotolewa leo jijini Dar esalaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Muhandisi Musa Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara
hiyo zitafanyika tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda
ya Kawe kuanzia saa nne asubuhi.
Taarifa hiyo
imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa
kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano
wa magari katika jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment