Habari zilizofika Uwazi kuhusu mkasa huo zinasema, Happiness aliyekuwa akiishi na shangazi yake, alipotea Agosti 27, mwaka huu baada
ya kuaga kuwa anakwenda saluni kupunguza nywele na hakurudi tena hadi
siku iliyofuata mwili wake ulipookotwa ukiwa umeanza kuharibika.
Tukio hilo la kinyama lilmegusa
hisia za wakazi wengi wa Manispaa ya Shinyanga hasa ikizingatiwa kuwa
mwishoni mwa mwaka jana, muuza urembo mmoja alikamatwa kwa tuhuma za
kuwabaka na kuwatoboa macho wanafunzi wanne wa shule za msingi za
Manispaa ya Shinyanga. Mtuhumiwa huyo alihukumiwa kifungo cha maisha
jela.
Baadhi ya watoto walioathirika
katika matukio ya ubakaji uliofanyika katika maeneo tofauti ya Mji wa
Shinyanga walilazwa kwa muda mrefu katika hospitali ya mkoa na wengine
kupelekwa Bugando jijini Mwanza lakini hata hivyo, baadhi yao macho yao
yameathirika.
Kwa mujibu wa maelezo ya mlezi wa
mtoto Happiness, John Njai ambaye ni mume wa shangazi yake, siku moja
kabla ya tukio, marehemu aliomba shilingi mia tano kwa ajili ya kunyolea
nywele.
Baada ya kupewa hela hiyo inadaiwa
bibi yake alimtaka anyoe nywele hizo nyumbani ili fedha hiyo itumike kwa
matumizi mengine, lakini alikataa kwa madai kuwa angenyolewa vibaya na hivyo kuchekwa na wenzake shuleni.
Bibi huyo alimruhusu mjukuu wake
kwenda saluni na kwamba akiwa njiani anarudi aliomba lifti kwa watu
wawili waliokuwa kwenye baiskeli moja lakini walimnyima kwa madai ya
kukosa kiti cha nyuma.
Baada ya kuchelewa kurudi nyumbani, wazazi na walezi walipata wasiwasi hivyo
kuanza kumfuatilia kwa ndugu na majirani, lakini hawakufanikiwa licha
ya kutoa tangazo msikitini juu ya kupotea kwa binti huyo.
Pia walitoa taarifa kwa mwenyekiti
wa mtaa, Kituo cha Polisi cha Nkomo na kwa ndugu na jamaa wanaowafahamu
na hatimaye Agosti 28, mwaka huu,
mtu mmoja alisema mwili wa mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka
tisa au kumi umeokotwa katika Kijiji cha Nhelegani ukiwa umeharibika.
Polisi waliuchukua mwili huo kwa ajili ya uchunguzi, baadaye waliruhusu mazishi yake huku hofu na simanzi zikiwa dhahiri kwenye nyuso za ndugu, jamaa na marafiki. Hapiness alizikwa katika makaburi ya familia yaliyoko kijijini Negezi.
No comments:
Post a Comment