Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela
miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba
nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Hukumu
hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara
baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya(cables)
za kampuni ya TTCL zenye thamani ya shilingi milioni 15.
Awali akisomewa shitaka hilo, Muhidin Ndina anadaiwa kutenda kosa
hilo Januari 11, 2013 maeneo ya Boko Katika Wilaya ya Kinondoni kabla ya
kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi namba 12/2013.
“Aliiba nyaya (cables) za thamani ya milioni 15 alitenda kosa hilo
Januari 11, 2013 Boko Katika eneo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam ”
ilisomeka sehemu ya hukumu ya kesi hiyo.
Uharibifu wa miundombinu ya umma zikiwemo nyaya za simu za Kampuni ya
TTCL umekuwa ukishamiri maeneo kadhaa jambo ambalo limekuwa
likisababisha hasara kubwa kwa kampuni na usu mbufu kwa wananchi na
watumiaji wa huduma za TTCL.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment