JUMBA lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya washiriki wa shindano la Big
Brother Africa (BBA) 2014 limeteketea kwa moto jana eneo la Sesani
Studios jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha uzinduzi wa shindano hilo kwa
mwaka huu kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kufanyika
Jumapili ijayo ya Septemba 7, mwaka huu.
Katika taarifa iliyotolewa na waandaaji wa shindano hilo, M-Net na
Endemol ni kwamba katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na chanzo cha
moto huo bado hakijafahamika huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo
chake.Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa sasa linatafutwa jumba lingine litakapoendeshwa shindano hilo linalochukua siku 91.
No comments:
Post a Comment