Kocha mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola
amezua majibizano makali baada ya kudai kuwa Manchester United hawana
pesa za kutosha kuwashawishi wachezaji wake kutoka Allianz Arena. Man
chester united imetumia takriban pauni milioni £150m kuwanunua
wachezaji akiwemo mchezaji aliyeghari9mu kitita kikubwa zaidi nchini
Uingereza Angel Di Maria kutoka Real Madrid.
Maria aliigharimu United takriban pauni milioni £59.7m alipotua Old Trafford.Sasa Guardiola akizungumza na wanahabari alisema kuwa hana hofu ya kuwapoteza wachezaji wake kwenda Old Trafford. "hawana pesa .
Samahani hawana hela hawa ''
Kocha huyo mwenye umri wa miaka $£ alinukuliwa akisema .
Guardiola, alikuwa akizungumza kabla ya mabingwa hao wa Bundesliga kuchuana dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester City .
''Niliwaona wakitumia pesa nyingi tu lakini unajua hawa wachezaji wnyewe wameamua kusalia hapa tu ''
Guardiola, aliwahi hudumu chini ya Louis van Gaal' alipokuwa Barcelona kabla ya wawili hao kutengana Pep alipoondoka kuchukua wadhfa wake mpya kama kocha.
No comments:
Post a Comment