Elizabeth Michael ‘Lulu’ akifurahia jambo.
Staa wa
Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni alijikuta
kwenye wakati mgumu baada ya mapedeshee wa Bukoba kumganda na kumzonga
huku kila mmoja akitaka namba yake ya simu.
Staa wa Filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisherehesha.
Lulu
aliongozana na wasanii wengine akiwemo Kulwa Kikumba ‘Dude’ kwenye
uzinduzi wa hoteli iitwayo Nalfin iliyozinduliwa juzikati wilayani
Muleba ambapo staa huyo alionekana kuwaumiza vichwa wanaume wakware
wenye fedha zao.
Chanzo
chetu kilichokuwa eneo la tukio kilidai kuwa, kutokana na jinsi Lulu
alivyowatikisa mapedeshee hao, baada ya uzinduzi, wanaume walimzonga
huku wengine wakitaka mawasiliano ambapo Dude alilazimika kumuokoa kwa
kugeuka baunsa.
Lulu
hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo ila Dude alipopatikana
alisema: “Ni kweli alikuwa na wakati mgumu, si unajua tena! Nililazimika
kugeuka baunsa wake maana walimzonga.”
No comments:
Post a Comment