Rais Jakaya Kikwete,
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa
kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio
linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Bunge hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu
ya katiba mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya
Kamati ya Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba
inayopendekezwa iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.
Katiba hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe
kutoka vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa
chama tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi
mbalimbali yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga.
No comments:
Post a Comment