Lorraine
Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja
wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano
ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20
bora.
Na Andrerw Chale
MWANADADA
Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo
ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika
nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok,
Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na
kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza
na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine
aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye
mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline
Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka
huu.
“Pongezi
kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya
Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha,
Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Lorraine
Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI,
alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand
International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Katika
mapokezi hayo, Lorraine alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na
mtendaji Mkuu wa Redline Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau
wengine walijitokeza uwanjani hapo.
Kwa
upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru
watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya
Tanzania.
Hii
ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa
hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd,
ambapo mshiriki wake huitwa ‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu,
Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top
Models 2013.
Aidha,
Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba,
ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot
Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano
hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika
nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu,
ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na
thamani za ndani.
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
No comments:
Post a Comment