Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za
Afrika-Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka
za mkutano wa kundi
namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao
umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa
Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia
Mkutano
wa
kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila
mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la
nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni
shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi
zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.
Katika
mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala
kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali.
Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti
atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi
hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri
wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi
kattika Benki ya Dunia.
Akiongea
katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza
la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka
Zimbabwe “ alisema.
Akiendelea
kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake
anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila
nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza..
Vilevile
katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti
ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion.
Jambo
lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki
itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa
IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.
Vilevile
walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea
kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo
tatizo.
Pia Benki
ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi
kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu
kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia
ujuzi wanao upata.
Mwisho
walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga
matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya
BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa
sasa.
Hali ya
hewa mjini hapa ni baridi kiasi.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington
D.C
9/10/2014
No comments:
Post a Comment