Picha za waandamanaji wakielekea kituo cha polisi.
KAMERA ya
GPL imewashuhudia wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wakiandamana
kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani, baada ya kudai kuwa
ndugu zao wamekamatwa wakiwa hawana makosa na kupelekwa kituoni.
Wakizungumza
na GPL baadhi ya waandamanaji walisema difenda tano za Polisi
zilikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu ovyo kwa madai kuwa ni
wahuni na wavuta bangi.
Dereva
mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao hufika na kuwakamata
wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya uhalifu, ila
kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi wakaaanza
kukamata watu hovyo hata wasiohusika.
No comments:
Post a Comment