HATARI!
Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja aliyefahamika kama Mama Abuu
amefanya tukio la ajabu baada ya kumng’ata na kumkata ulimi kijana Paulo
Simon mwenye umri wa miaka 18, kufuatia ‘Serengeti Boy’ huyo kukataa
kufanya naye mapenzi katika eneo la Tindigani, Kimandolu mjini Arusha
hivi karibuni.
Meru
jijini hapa, alisema alikuwa akiuza baa katika eneo hilo wakati mwanamke
huyo alipotokea na kukaa kaunta na kuanza kunywa pombe kama wateja
wengine. Alisema ilipofika saa 6:30 usiku wateja wengine wote waliondoka
na kubakia mama huyo pekee, kitu kilichomfanya naye afunge baa. Lakini
alipomaliza kufanya hivyo mama huyo alimfuata na kumweleza kuwa
alihitaji kufanya naye mapenzi.
Alisema
baada ya kukatwa ulimi ambao sasa unamletea maumivu makali, alifanikiwa
kufika nyumbani kwake kabla ya tajiri yake kumchukua na kumpeleka
hospitalini ambako amelazwa.
Jeshi la
Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni huku uchunguzi ukiwa unaendelea. Hali ya
majeruhi inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment