Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi
ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kushoto ni
Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa
Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw.
Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya
Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa
utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani
nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na mwandishi wetu, Dodoma
Naibu
Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo
katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja
zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio
waathirika wakubwa wa ajali.
Aidha
amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji
wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na
kuondoa tuhuma za rushwa.
Kauli
hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na
watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya
siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga
kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao
iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia maendeleo (UNDP).
washa
ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga
kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph,
akisalimiana na Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi
Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili
kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment