HUKU
mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili
Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia
madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa
kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano
linateremka nayo.
WATOA MADAI
Hivi
karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers
na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa
akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo
za Injili.
“Sisi
tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine wanasema
sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya awe kama
amelewa na kushindwa kufanya lolote.
“Huwa
anafika hatua anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo
maana mtu anaweza kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa
kutoka ndani kwake.
No comments:
Post a Comment