Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigala(mwenye suti nyeusi)pamoja na
Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City (kushoto)wakionesha hundi yenye
thamani ya Tsh Milioni 1/= kwa mashabiki wa timu yake mara baada ya
kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa wilaya hiyo kwa niaba ya wadhamini wakuu
wa ligi kuu Vodacom Tanzania hapo jana kabla ya mechi kuanza baina ya
timu Mbeya City na Azam FC,Ambapo Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli
moja bila na anaeshuhudia kulia ni Katibu wa chama cha mpira wa miguu
mkoa wa Mbeya(MREFU) Seleman Harub.
Mchezaji
bora wa mwezi Septemba wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara wa timu ya
Mbeya City Anthony Matogolo akiwaonesha mashabiki wa nyumbani Ngao
aliyokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr.Norma
Sigala(kushoto)kwa niaba ya wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania
pamoja na hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 1/= kabla ya kuanza kwa
mechi kati ya timu ya Azam FC na Mbeya City hapo jana/juzi ambapo Azam
FC iliilaza Mbeya City goli moja bila.
Mtanange ukiendelea katika ligi kuu ya vodakom katika Uwanja wa Sokoine.
Wachezaji
wa timu ya Azam FC wakishangilia goli lao lililofungwa na Aggrey
Morris katika mzunguko wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu
hiyo na Mbeya City hapo jana/juzi Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli
moja bila.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
WADHAMINI wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kampuni
ya Huduma za Mawasiliano ya Vodacom imekabidhi zawadi ya Sh. milioni
moja kwa mchezaji bora wa mwezi uliopita wa ligi hiyo, Antony Matogolo
wa Mbeya City.
Makabidhiano
hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya nne kati ya
Mbeya City na Azam FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa
jana.
Kabla ya kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Vodacom Tanzania Kanda ya
Mbeya, Emmanuel Sagenge, alisema kampuni hiyo itakuwa ikitoa zawadi kila
mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.
“Ligi Kuu ya
Vodacom msimu huu ina ushindani mkubwa, nasi (Vodacom Tanzania) kwa
kushirikiana Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) tutakuwa tunatoa zawadi kwa
mchezaji anayeng’ara kila mwezi na leo (jana) tunatoa Sh. Milioni moja
kwa Antony Matogolo,” alisema Sagenge.
Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Mtogolo aliyeonekana mwenye
furaha,alisema; “ninawashukuru wachezaji na mashabiki wa Mbeya City kwa
ushirikiano wanaonipa, hii ni zawadi kwa timu nzima na mashabiki wa timu
yetu.”
Aidha,
wadau wa Mbeya City waliungana na Vodacom Tanzania katika hafla hiyo ya
utoaji zawadi na kukabidhi zawadi ya fedha kwa kocha bora msimu
uliopita, Juma Mwambusi wa Mbeya City huku wakitoa fungu pia
kwa Matogolo.
Matogolo
aliiongoza Mbeya City katika mechi mbili za mwezi uliopita walitoka
suluhu dhidi ya JKT Ruvu Septemba 20 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya
Coastal Union Septemba 27.
Katika mechi ya jana, Mbeya City ilifungwa goli 1-0 dhidi ya mabingwa
watetezi Azam FC. Goli la Wanalambalamba lilifungwa na beki wa kati
Aggrey Morris kwa shuti kali la faulo dakika nne baada ya robo saa
ya mchezo.
No comments:
Post a Comment