Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Tanzania Salum Mwalim,akiongea na waandishi wa habari(hawapo
pichani)wakati wa kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom. kushoto ni Meneja biashara wa TFF Peter Simon na kulia ni
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga.Timu 14
zimekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh 430 Milioni.
Kutoka kushoto: Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Bodi ya ligi Silas Mwakibinga,Mwakilishi wa klabu ya Azam FC Phillip
Alanzo na Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakionesha jezi za Azam FC
walizokabidhiwa na mdhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom kampuni ya Vodacom
kwa ajili ya msimu wa 2014/2015. Timu 14 zimekabidhiwa vifaa vyenye
thamani ya zaidi ya Sh 430 Milioni.Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Tanzania Salum Mwalim(kushoto) akimkabidhi jezi Mwakilishi wa
JKT Ruvu akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi Silas
Mwakibinga(katikati) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa
timu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.Vifaa hivyo zimetolewa na
wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.Kutoka kushoto: Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa
bodi ya ligi Silas Mwakibinga,Mwakilishi wa timu ya Kagera Sugar na
Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakionesha jezi ilziokabidhiwa timu ya
Kagera kwa na kampuni ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2014/2015.
Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14 zinazoshiriki ligi hiyo.Mwakilishi wa timuu ya Mbeya
City akipokea kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania
Salum Mwalim(kushoto) jezi zitakazotumiwa na timu hiyo katika msimu wa
2014/2015 wa ligi kuu ya Vodacom. Wa pili toka kusho ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF
Geoffrey Nyange .Vodacom imekabidhi vifaa kwa timu zote 14
zitakazoshiriki ligi kuu vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni
430.Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Silas
Mwakibinga na kulia ni Mjumbe wa TFF Geoffrey Nyange wakifurahia jambo
pamoja na Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto wane toka kushoto
wakati wa hafla ya Vodacom kukabidhi vifaa kwa timu 14 zitakazoshiriki
Ligi Kuu ya Vodacom.AfisaMendaji Mkuu wa bodi ya
ligi Silas Mwakibinga(katikati)akipokea vifaa vipya toka kwa Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, vitakavyotumiwa na
waamuzi katika mechi mbalimbali za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara
zitakazoanza hivi karibuni. Jumla ya zaidi ya shilingi Milioni 430
zimetumika katika kununua vifaa kwa timu 14 zitakazoshirikii Ligi Kuu ya
Vodacom 2014/2015 pamoja na vifaa vya waamuzi.
No comments:
Post a Comment