LEneo la makaburi ya Musima Bus walipozikwa baadhi ya marehemu wa ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express iliyotokea wiki iliyopita.
UMATI wa watu jana umejitokeza katika
makaburi yaliyopo jirani na stendi ya Musa Mabasi, mjini Musoma baada ya
kubaini kuwa kaburi mojawapo kati ya yale waliyozikwa marehemu wa ajali
ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wiki iliyopita limefukuliwa na
mwili wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Mzee Swai ukiwa nje na hauna
baadhi ya viungo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, mwili
huo ulikuwa hauna baadhi ya viungo vya sehemu za siri kitendo kilichozua
hasira kwa wananchi hao na kuwalazimu polisi kuingilia kati
kuwatawanya.
Baada ya kuwatawanya wananchi hao, polisi
walifanya uchunguzi kisha kushirikiana na baadhi ya wananchi hao kuuzika
tena mwili wa mzee Swai huku wakiahidi kufanya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment