Mwimbaji wa Bongo Flava, Rich Mavoko amewataka wasanii wa Tanzania
kukumbuka mchago wa mtayarishaji mkongwe wa videos za muziki nchini Adam
Juma pale wanapofikiria kuhusu kiasi cha kumlipa.
“Analipwa kawaida, analipwa vilevile tu.” Ameongeza.
Akiongea na tovuti ya Times Fm Rich Mavoko ambaye anatarajia kuachia
video mpya ya wimbo wake ‘Pacha Wangu’ aliyoifanya Cape Town, Afrika
Kusini na kuongozwa na Adam Juma amewataka wasanii wasilalamike kuwa
Adam Juma anahitaji pesa nyingi ya kufanyia video bila kukumbuka uwezo
wake na mchango wake.
“Lakini tuangalie pia ametutoa wapi. Movement zake kuhusu music video
Adam Juma ameitoa wapi. Tuapreciate kitu ambacho amekifanya. Mimi naweza
nika-appreciate media, maDj, na wasanii wenzangu basi tuapreciate pia
(Adam J) ametutoa mbali ujue.” Rich Mavoko ameiambia tovuti ya Times
Fm.
Akizungumzia kuhusu video yake, ameeleza kuwa Adam Juma alisafiri na
crew yake yote na alitumia vifaa vya kisasa kukamilisha kazi nzima Cape
Town.
No comments:
Post a Comment