Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally
‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar
akihusishwa
na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa
kipigo ambapo inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.Msanii wa Muziki wa Bongo
Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa
Polisi. Baada ya tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita,
Ijumaa lilinasa picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni
hapo huku mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa,
licha ya ustaa wake Madee alikiona cha mtemakuni.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni, nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka mahakamani.
“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila inavyodaiwa baadhi
ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru baada ya kulala
selo,” kilidai chanzo hicho.
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na
Madee. Kufuatia msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake
Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua
simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe
ndipo Madee alipomtaiti Suedi na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa
polisi kwa kufunguliwa kesi iliyosomeka:VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA
BINADAMU
Imeandikwa na Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani na Rhoda Josiah.
No comments:
Post a Comment