Sakata la mtoto aliyezamia ndege kutoka Dar es Salaam kwenda
Zanzibar, Karine Godfrey (ambaye sasa imefahamika kwa jina la Happiness
Rioba )limechukua sura mpya baada ya mama yake mzazi, Sara Zefhania
kujitokeza na kusema kuwa mwanaye hakupanda ndege.
Akizungumza na gazeti hili jana, Zefhania ambaye
ni mkazi wa Mkokozi Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani alisema Karine
hakupanda ndege ila alipotea.
Alisema mtoto huyo ana tatizo la kutoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha na kwamba hata safari hiyo ilikuwa na utata
Alisema kuwa hata majina aliyotumia siyo majina
yake halisi kwani anaitwa Happines Rioba na kwamba hakupanda ndege
isipokuwa ni yale mazingira yake ya utata ambayo amekuwa akitumia.
Alifafanua kuwa tabia hiyo ya kutoweka kwa mtoto ilianza mwaka
2010 ambapo alitoweka nyumbani kwa kipindi cha mwezi mmoja na
alipatikana mkoani Mwanza akiwa katika mazingira yasiyoeleweka.
Aliongeza kuwa madai ya kusema kuwa alisindikizwa
na dada yake kwenda kupanda ndege siyo ya kweli ila ni yeye mwenyewe
kutokana na tabia hiyo ya kutoweka na kwenda kusikojulikana.
Alisema mwanaye huyo amekuwa akitoweka nyumbani
mara kwa mara kitendo ambacho kinafanya maendeleo ya shule kuwa mabaya
na wakati mwingine amekuwa akirudishwa darasa.
Alisema kwa kipindi chote tangu atoweke nyumbani
alikuwa akimtafuta sehemu mbalimbali bila ya mafanikio na kwamba jana
(juzi) alipata taarifa kuwa mwanaye ameonekana Zanzibar kuwa alionyeshwa
katika ITV.
Aliongeza kuwa anapotoweka huwa anatoa taarifa
Polisi na kwamba anasoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Kelezange
iliyopo Kitunda na siyo Shule ya Jitihada kama alivyodai mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment