Bunge Maalumu la Katiba linaeelekea ukingoni.Yapo mambo mengi yaliyofanywa kuhusu Mchakato wa Katiba ndani na nje ya Bunge hilo.
Mathalani katika shughuli za Bunge kulikuwa na
idara na taasisi kadhaa ambazo bila ya uwepo wake kazi nzima isingeweza
kufikia mahali hapa sasa.
Miongoni mwa idara hizo ni Habari na Itifaki
ambayo kazi yake kubwa ndani ya bunge hilo ilikuwa ni kufanya shughuli
zote za uratibu wa namna habari za bunge hilo zitakavyowafikia wananchi.
Vyombo mbalimbali vya habari vilituma wawakilishi wao katika
Bunge hili ambao wamefanya kazi ya kupeleka kwa jamii kila kilichotokea
ndani ya jengo hilo licha ya kuwa baadhi ya mambo watawala waliyapinga.
Oweni Mwandumbya ni mtumishi wa Bunge katika idara
ya Habari na Itifaki ambaye wakati wote amekuwa karibu na vyombo vya
habari na wanahabari katika kuhakikisha shughuli zao zinafanikiwa.
Akiwa ofisini kwake anazungumzia namna ambavyo
kazi hiyo ilikuwa na msisimko mkubwa na jinsi jamii na wanahabari
walivyomfanya akose usingizi wakati wote. Fuatilia mahojiano yake hayo
na gazeti na gazeti hili:
Swali: Idara ya habari mmekuwa ni sehemu ya bunge
hili, lakini muda mwingi hamuonekani kabisa na mnapoonekana ni pale
ambapo mnabebeshwa lawama, nini mchango wenu?
Jibu: Ni kweli, unaweza kuona kama hatupo vile
lakini ukweli ni kuwa bila ya idara hii pamoja na wanahabari wake,
Watanzania walio wengi wasingeona kila kinachoendelea.
Swali: Kazi yenu ni nini hasa katika Bunge la Katiba?
Jibu: Kazi yetu ni kuratibu, kusimamia na
kushughulikia masuala yote ya habari za Bunge la Katiba na kuhakikisha
tunafikisha ujumbe kwa jamii.
Kazi nyingine ni kuweka mazingira ambayo
yatamwezesha mwandishi wa habari wa Bunge la Katiba kufanya kazi yake
kwa ufanisi bila wasiwasi.
Swali: Nani ni mwandishi wa habari za Bunge maalumu a Katiba, au kila mtu anaweza kuandika habari za Bunge hili?
No comments:
Post a Comment