Maafisa
wa utawala nchini India, wanachunguza ambavyo kitambulisho cha
elektroniki kimetengezwa kikiwa na picha ya Hanuman mungu wa kihindi na
kutumwa kwa njia ya posta.Kitambulisho
hicho kina picha ya mtu anayejulikana kama Hanuman kutoka kwa kipindi
kilichojuolikana kama Ramayana, akiwa amevalia mikufu ya dhahabu na taji
la kifalme.Kitambulisho chenyewe kilipatikana wakati mfanyakazi wa
posta alijaribu kukifikisha kwa mtu aliyetumiwa ila hangeweza kupata
anwani ya mtu yeyote anayejulikana kama Hanuman.
Alipoangalia
kwa picha , aligundua kuwa huenda ilikuwa mchezo wa danganya toto. Bado
haijaulikana ni nani aliyeweka alama ya kidole kwenye kitambulisho
hicho.
Hanuman alijulikana kama mtoto wa mungu wa kihindi
aliyejulikana kama Pawan, na kitambulisho chenyewe kina namba ya simu na
anwani ya sehemumoja katika jimbo la Rajasthan. Hanuman alijulikana
kama mungu wa kihindi mwenye nguvu za ajabu na mtiifu sana
Kwa kawaida Hanuman huonekana akiwa na uso wa Nyani pamoja na mkia. Kuna hekaya za kale kuhusu Hanuman kote nchini India.
Mfanyakazi
huyo wa posta Heeralal Saini, alikirejesha kitambulisho hicho kwenye
kituo cha posta baada ya kukosa kumpata mtu kwa jina la Hanuman.
'Hanuman ni nani?'
Hanuman
ni mmoja wa miungu wanaobudiwa na watu nchini India na pia kuna hekaya
nyingi tu kwenye vitabu vya kihindi kumhusu. Huonekana kama binadamu
mwenye uso wa Nyani na mkia mrefu.
Mara kwa Mara yeye husemekana
kuwa mtoto wa mungu mwingine wa kihindi Pawan na anasifika kwa kuwa
mtiifu na mwaminifu pamoja na kuwa na nguvu
No comments:
Post a Comment