Geita. Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme
(Tanesco) Mkoa wa Geita, wa Geita, Charles Budodi juzi alijikuta kwenye
wakati mgumu, baada ya kushindwa kujibu maswali yaliyoelekezwa kwake na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele kuhusu shirika hilo
kukaidi agizo la Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha shirika hilo linapeleka
umeme kwenye shughuli za wachimbaji wadogo.
Hali hiyo ilijitokeza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita, alipowasili kijijini
hapo kuzindua mgodi wa mfano wa wachimbaji wadogo. Alipofika eneo hilo,
naibu huyo alikuta maeneo ya wachimbaji wadogo hayana huduma ya umeme
licha ya umeme kufikishwa katika kijiji hicho,
Masele alionyesha kukerwa na kitendo hicho cha kukaidi agizo la
Rais, huku wananchi waliokuwa mkutanoni hapo wakimzomea kaimu meneja
huyo kwa kumwomba naibu waziri kuondoka naye wakidai ametoa majibu ya
uongo.
Masele.”Meneja yuko wapi…Tuambie kwa nini umeme
haujafika kwa wachimbaji wadogo, wakati tayari Rais aliagiza umeme
upelekwe huko? Umefanya utafiti ni wachimbaji wangapi wanahitaji umeme”
Meneja, ”Mheshimiwa, tumefanya tathmini na tumezunguka Nyarugusu na hapa Lwamgasa, tutaleta umeme.”
No comments:
Post a Comment