Msiba! Bado bundi wa vifo anaendelea kung’ang’ania tasnia ya sinema za Kibongo kufuatia kifo cha ghafla cha msanii wa Bongo Muvi, Mariam Juma ‘MC Chimamy’ ambaye amefariki dunia ghafla baada ya kupatwa na kifafa cha mimba, ugonjwa uliomkuta muda mfupi kabla ya kujifungua.
Mauti
hayo yalimkuta MC Chimamy wikiendi iliyopita baada ya kukimbizwa kwenye
Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, akiwa tayari na hali mbaya kwani
kabla ya hapo alianzia
Hospitali ya Palestina, Sinza ambapo alilazimika kukimbizwa katika
hospitali hiyo ya Wilaya ya Kinondoni ili kunusuru maisha yake na kiumbe
alichokuwa nacho tumboni.
Msiba huo umezua simanzi kubwa kwa
wasanii wenzake hasa Vanita Omary, Halima Yahya ‘Davina’, Yvonne-Chery
Ngatwika ‘Monalisa’, Mariam Kakwaya na wengine kwani alikuwa ni mtu wao
wa karibu na siku
aliyokutwa na umauti alikuwa amepangwa kuwa mshereheshaji wa shughuli
ya Davina ya kibao kata iliyofanyika Bamaga-Mwenge, Dar.
“Msiba huu umenishtua sana, sikutarajia kama Chimamy angetutoka kimchezo hivi, ukweli nimeumia sana na sina la kusema, namshukuru Mungu kwa kazi yake,” alisema Vanitha.
No comments:
Post a Comment