Dar es Salaam. Zaidi ya waathirika 1,300 wa
mabomu yaliyolipuka Mbagala na kusababisha vifo na uharibifu wa mali,
wamemwomba Rais Jakaya Kikwete kuwasaidia ili wapate fidia ya mali zao
kama alivyokuwa ameahidi alipowatembelea.
Mabomu hayo yalilipuka Aprili 29, 2009 katika
Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) KJ 671 na kusababisha vifo vya watu
zaidi ya 20, huku mamia wakijeruhiwa na familia nyingi kukosa makazi
baada ya nyumba zao kubomoka kabisa.
Wakizungumza jana, walisema kuwa Serikali inapiga
‘danadana’ suala lao, wakati idadi yao inazidi kupungua, kwani tangu
wameanza kufuatilia fidia hiyo, wenzao 17 wameshafariki dunia kabla ya
kupata haki zao.
Mwenyekiti wa waathirika hao, Steven Gimonge alisema kuwa ingawa
Rais Kikwete alipowatembelea baada ya tukio hilo aliwaambia kuwa
watalipwa hata vijiko vilivyo haribika, baadhi yao wamelipwa hundi za
Sh1,400 na Sh1,950.
Kutokana na malipo hayo kuwa kidogo, walimwandikia
barua Rais Kikwete Machi mwaka huu wakitaka waandamane, lakini
walizuiwa kwa madai kuwa suala lao linashughulikiwa.
“Tunaambiwa tu subiri subiri; subiri hii mpaka
lini hata kama alikuwa mtu amebeba mimba angekuwa ameshazaa na mtoto
ameanza shule…au walitutoa kafara?
“Rais Kikwete agundue kwamba kumbe kuna
wanaMbagala niliowaahidi watalipwa hadi kijiko kumbe hawajalipwa
kabisa,” alisema Gimonge.
Aliongeza kuwa baada ya mlipuko wa mabomu,
Serikali na wadau wengine walipeleka fedha, lakini katika hali isiyokuwa
ya kawaida haijulikani ni nani aliyepewa.
“Vitu vililetwa yakajaa madarasa mawili, saruji tani 2,500, mabati tani 2,500 na magodoro, hatukupewa hata mtu mmoja.
“Kama tunavyosema sisi ni yaya (msichana wa kazi)
amekula akifikiria kwamba mtoto amekula, kumbe sivyo. Tunamwomba Rais na
wapenda amani duniani watuunge mkono, hata kama hela zilitolewa na
wafadhili sisi hatukupewa, walikula wenyewe,” alisema.
Akishuhudia namna mabomu hayo yalivyomwathiri
kiafya, Mwenyekiti huyo alisema kuwa alipata kifua kikuu mara mbili na
kwamba hivi sasa anatibiwa saratani ya kibofu.
Kuhusu malipo
No comments:
Post a Comment