MAGONJWA
YA MOYO BADO NI MIONGONI MWA MAGONJWA YANAYOCHANGIA VIFO VINGI TANZANIA
Dar es Salaam, Septemba,
2014. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO zilizotolewa
mwaka 2011, Vifo vilivyotokana na magojwa ya moyo nchini Tanzania vilifikia idadi ya watu 19,083, au asilimia
4.33% ya idadi ya vifo vyote. Na takwimu hizo zilionyesha idadi ya wanaofariki
ni watu 117.64 kati ya watu 100,000, na takwimu hizi zikiiweka Tanzania katika
nafasi ya 87 ulimwenguni.
Magonjwa haya ya moyo yanasababisha vifo
vipatavyo idadi ya watu milioni 12 kwa mwaka duniani kote. Hata hivyo shirika
la Afya Duniani limekua likifanya jitihada za lazima za kujaribu kupunguza vifo
vitokanavyo na magonjwa ya moyo na sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo.
Magojwa haya ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kiharusi, shinikizo la damu , ugonjwa wa pembeni wa mishipa ya moyo, , ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa na moyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Katika kuonyesha kukua kwa maendeleo ya kiteknolojia ya huduma za afya, Hospitali ya Apollo ya mjini Gujarat , katika mji wa Ahmedabad, ilifanikiwa kufanya upasuaji unaojulikana kitaalam kama ‘Bentall Surgery’ kwa mwanamke aliyekuwa na zaidi ya miaka 50. Upasuaji wa aina hii mara nyingi ni adimu kufanyika katika nchi ambazo ni masikini na zenye wataalamu wachache, ama zenye mfumo wa chini wa huduma za afya. Upasuaji huu uliofanywa kwa mwanamama kutoka Tanzania, uliukuwa ni wa aina yake, na ulichukua muda wa saa saba. Hii inaonyesha jinsi gani hospitali hizi zilivyo na uwezo Na utaalam wa hali ya juu.
Mama huyo alikuwa akilalamika toka maka 2009
kuhusu maumivu ya mgongo, na alipofanyiwa uchunguzi wa kina, ilionekana kuwa
alikua na matatizo katika moyo wake, ambayo hata hivyo hayangeweza kutibiwa hapa
nchini. Alipelekwa katika hospitali ya Apollo ya mjini Ahmedabad, hospitali
inayosifika kwa kufanya upasuaji kwa ufasaha na uhakika zaidi.
Mama huyu alifanikiwa kufanyiwa upasuaji huo
mgumu wa moyo uliochukua zaidi ya masaa saba, ilionekana kuwa alikua na
matatizo makubwa katika mishipa ya Aorta ambayo yalisababisha moyo wake
ushindwe kufanya kazi kama kawaida. Hatimaye upasuaji huo ulifanikiwa, na
pengine asingeweza kupona kama bado angelikuwapo nchini hapa, na hali yake
inaendelea vizuri.
“ katika masuala ya afya, bara
la Afrika liko kama bara la Asia miaka 25 ama 30 iliyopita. Wale tu wenye
kipato cha juu ndiyo wanaoweza kumudu huduma za uhakika nje ya nchi’’, Anasema Dr Hari Prasad, mkurugenzi mtendaji
wa hospitali za Apollo.
"Ni wakati muafaka sasa wa kutumia uwezo wetu na utaalam
wetu kuwatibu wenye matatizo. Tulichoifanyia india hatuna budi kuifanyia dunia
na nchi zinazoendelea, Anaongezea Dr Pratap
C Reddy, mwenyekiti wa hospitali wa za Apollo Mbali na Tanzania, Hospitali
ya Apollo imepania kukita mizizi yake katika nchi mbalimbali za Afrika , ambako
imekua ikipokea idadi ya wagonjwa wengi kutoka bara hili, na ina matarajio ya
kuanzisha vituo kadhaa vya Afya katika eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika
magharibi hapo mbeleni.
Zaidi kuhusu hospitali za apollo
Hospitali
ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa
ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa
karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika
elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".
No comments:
Post a Comment