Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata
alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake
aliyefariki dunia juzikati.Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akiwa
mamtoni. Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za
mdogo wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye mazishi.
K.Y ilipata bahati ya kuwasiliana na Aunt ambaye alisema ameshitushwa na taarifa hizo na alikuwa njiani kurejea Dar.
“Nimeumia sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu tuliyependana sana
lakini Mungu kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa masikitiko.
No comments:
Post a Comment