Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema
hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa kuwa amemlea
na amemesaidia vitu vingi zikiwamo fedha, gari, kula na kulala nyumbani
kwake.Mbowe alisema Chadema hakijamtenga Zitto bali alijitenga mwenyewe
na kufafanua kuwa Chama hicho hakiwezi kujengwa na viongozi ambao ni
wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyasema
hayo jana katika Kata ya Kalinzi, Jimbo la Kigoma Kaskazini katika
ziara zake za ‘operesheni delete CCM’ kuelimisha wananchi kuhusiana na
uchaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa.
Mbowe
alisema hayo baada ya kuruhusu maswali kutoka kwa wananchi ndipo Cheche
wa Cheche alipomuuliza kwamba kwa nini Zitto hayumo katika ziara hiyo
wala ya Katibu Mkuu, Dk.Willibrod Slaa
“una
baadhi ya watu wanafikiri kuwa nampiga vita Zitto, siwezi kumpiga vita
Zitto kwa kuwa nimemlea, amekula na kulala nyumbani kwangu nami ndie
nilimshauri kugombea ubunge na kumpa fedha pamoja na gari, iweje leo
nimpige vita?” alihoji Mbowe wakati akijibu swali hilo.
No comments:
Post a Comment