Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Kikosi
cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua
jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa
Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam. Wachezaji
wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana
(Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) kwa nyakati tofauti. Kikosi
hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10
jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho
kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.Wachezaji
walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane Sessegnon (West Bromwich
Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon
(Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg,
Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed
Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve
Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne
63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia
Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na
Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean
Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef,
Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS
Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Nayo
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10
mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10
jioni.
Wakati
huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle
Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka
huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.
FDL YAANZA KUTIMUA VUMBI
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi
kesho (Oktoba 11 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya
Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es
Salaam.
Kundi
A litakuwa na mechi kati ya Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja
wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji itaumana na Ashanti United (Uwanja
wa Majimaji, Songea).
Nyingine
ni Kurugenzi Mafinga na Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku
Friends Rangers ikioneshana kazi na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B ni Panone itaikabili Kanembwa JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro
JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abedi,
Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Musoma).
Mechi
nyingine ni kati ya Toto Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa
CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita Gold na Burkina Faso (Uwanja wa
Waja, Geita).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment