Madee amezungumza kwa mara ya kwanza tangu apatwe na mkasa huo.
“Yule dogo baada ya kuniibia simu tulimgonga kwa nyuma akaanguka tukamwokota na kumbeba kwenye Noah yetu tukaondoka naye. Kesho yake nilikuwa na safari ya kwenda Mwanza kwahiyo nikaachia masela wampeleke polisi na hapo mimi nilishampigia simu mama yake ili aongee na mwanae aseme simu yangu iko wapi. Simu yangu yenyewe ndio ilikuwa kila kitu. Kwahiyo
nilivyoondoka
nikiwa sina hata mawasiliano, nikaenda Mwanza nimefanya show, nimerudi
Jumatatu asubuhi nikaulizia mtuhumiwa wangu nikaambiwa yupo Magomeni.
Nikaenda Magomeni polisi nikaambiwa dogo kahamishiwa Kigamboni,”
amesimulia Madee.
“Nikaamua kwenda Kigamboni, kwenda Kigamboni nikaambiwa ‘bwana wewe ndo unashtakiwa ukitaka kumteka huyu dogo’ ndio nikawekwa ndani, nikalala siku moja, asubuhi nikadhaminiwa nikatoka kesi ikaenda mahakamani. Mahakamani kesi ikaahirishwa siku ya kwanza siku ya pili ikapita, hukumu nikaambiwa kati ya kwenda jela miezi sita au kulipa faini 50,000. Nikalipa faini na kesi ikaisha. Yaani mimi ndo nimekuwa mwenye kosa, mimi ndo niliyelipa faini.”

No comments:
Post a Comment