Nyakiringa Stivin (39), mara baada ya kupigwa risasi tumboni. Kushoto kwake ni mkewe, Agness Lucas.
....wapita
njiawakijaribu kutoa msaada kwa mtu huyo.Global Publishers jana ilikuwa
ya kwanza kuripoti tukio la mwanamme mmoja kupigwa risasi maeneo ya
Magomeni Mikumi ambaye hakuweza kutambulika mara moja, lakini sasa
amejulikana na kwa taarifa zilizotolewa na ndugu, jamaa huyo amefariki
dunia leo afajiri akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marehemu ametambulika kwa jina la Nyakiringa Stivin (39), mkazi wa
Kibaha Picha ya Ndege na mwanamke aliyekuwa naye kwenye gari ameelezwa
kuwa ni mkewe, Agness Lucas. Marehemu ni fundi wa sofa na imeelezwa na
chanzo chetu kuwa alikuja jijini Dar kwa ajili ya kununua mahitaji yake
ya ufundi.
Alipopigwa risasi maeneo ya Magomeni alikuwa akitokea Access Bank
Manzese ambako alitoa fedha kiasi cha shilingi 12M. Kwa mujibu wa mkewe,
mkoba uliochukuliwa na majambazi ulikuwa na shilingi milioni 10 ambazo
zilibaki baada ya kufanya manunuzi maeneo ya Manzese.
No comments:
Post a Comment