Msanii Diamond (mwenye shati nyeupe) akiwa na Yamoto Band.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
WANAMUZIKI Diamond
na Yamoto Band wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Siku ya
Msanii litakalofanyika Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani
City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
leo katika ukumbi wa Maelezo , Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii (SYM) ,
Peter Mwendapole, amewataja wasanii wengine watakaokuwapo ni pamoja na
mwanamitindo Asia Idarous, Miss Tanzania, Miss Universe na wasanii toka
Kenya, Erick na Fred Omondi huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu
wa Rais, Gharib Bilal.
No comments:
Post a Comment