Habari
ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mtangazaji
mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM, Gardner G
Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ndiye
aeleze ukweli juu ya ndoa yao.
Mtangazaji
wa Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’ Akizungumza kwenye
Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia Televisheni ya EATV chini
ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne iliyopita, Gardner alikataa
kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika. Pamoja na mambo mengine
ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner alipoulizwa juu ya habari
zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika uhusiano wake na Jide au Lady
Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo kwamba kipindi hicho kilimhusu
yeye tu.
Mwanamuziki wa Bongo fleva kitambo, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
Mtangazaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia Salama kwamba amwite
Jaydee kwenye kipindi hicho ili alielezee jambo hilo kwa undani.Gardner
na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa
hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa
meneja wa mwanamuziki huyo yakielea.
Kupitia kipindi chake cha Diary of Lady Jaydee kilichokuwa
kikisimamiwa na Gardner ambacho sasa kinaongozwa na ndugu wa msanii huyo
aitwaye Wakazi, Jumapili iliyopita Jide alionekana kwenye harusi ya
ndugu yake aitwaye Lameck Mbibo ‘Dabo’ ambaye pia ni msanii wa Dance
Hall akiwa mpweke bila mumewe kama ilivyozoeleka.
No comments:
Post a Comment