Na Musa Mateja
Kufuatia tukio la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuonekana jukwaani na sare zinazoaminika kuwa za Jeshi la Wananchi (JWTZ) kisha kukamatwa kwa kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) na meneja wake, Babu Tale, kuna uwezekano wa jamaa huyo kufungwa jela miaka miwili au mitatu.
Kufuatia tukio la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuonekana jukwaani na sare zinazoaminika kuwa za Jeshi la Wananchi (JWTZ) kisha kukamatwa kwa kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) na meneja wake, Babu Tale, kuna uwezekano wa jamaa huyo kufungwa jela miaka miwili au mitatu.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akisubiri zamu yake kupanda jukwaani.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, baada ya jeshi kutoa
tamko kuwa ni kinyume cha sheria, juzi Diamond alitakiwa kwenda
kujisalimisha polisi lakini hakufanya hivyo jambo lililosababisha
wenzake kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Oysterbay,
Kinondoni jijini Dar.
Ilisemekana
kwamba baada ya Wasafi (madensa wa Diamond) kukamatwa, Babu Tale naye
alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi
walionekana katika eneo hilo wakiweka ulinzi mkali.
Madensa wa ‘Diamond Platnumz’ wa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) wakisindikiza shoo yake.
Chanzo
hicho kilieleza kwamba, siku ya tukio Oktoba 21, mwaka huu, uongozi wa
Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa 2:00 asubuhi lakini
haukufanya hivyo ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.
Hata
hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji kwa nini jeshi la polisi
lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vilieleza
kuwa mwanamuziki huyo huenda alikuwa safarini.
Diamond akiendelea kutoa burudani jukwaani.
Ilielezwa
kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni wanajeshi wa
Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni hapo kisha
kuendelea na mambo yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, Camillus Wambura alisema
bado hajawasiliana na kituo cha Oysterbay kuhusu suala hilo na hajapata
taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya Mkuu wa
upelelezi wa Mkoa.
Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
Diamond Chege wakifanya yao.
“Uchunguzi
unafanywa huko (Oysterbay). Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo
mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa. Sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika
uchunguzi wa suala hilo.”
Mapema
wiki hii, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilitoa taarifa kwa vyombo
vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
Kwa
mujibu wa mwanajeshi wa JWTZ ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si
msemaji wa jeshi hilo, taaluma yake ya sheria imemfanya kuchimba kwa
undani suala hilo na kugundua kuwa endapo Diamond atapatikana na hatia
atapigwa faini au kwenda jela miaka miwili au mitatu au vyote, yaani
faini na kifungo.
Alisema
kosa la Diamond ni kushindwa kutii wito kwani alitakiwa kuripoti
mwenyewe polisi hivyo lazima atapanda mahakamani kujibu shitaka hilo na
lile lenyewe la kutumia sare za jeshi hilo.Chanzo hicho kilidai kwamba
si mara ya kwanza kwa jamaa huyo kuingia kwenye kashikashi kama hiyo
kwani kuna kipindi alikwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
ambapo alionekana na sare hizo stejini na akapewa onyo lakini safari hii
amejiongeza tena kuonesha kuwa ni kichwa ngumu.
No comments:
Post a Comment